Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Uturuki: Raia wetu wawili wanaoshikiliwa Libya sio majasusi

media Wakaazi wa viunga vya mji wa tripoli wanaendelea kuyatoroka makaazi yao kufuati mapigano makali kati ya majeshi ya serikali na yale ya Marshal Khalifa Haftar. REUTERS/Hani Amara

Maofisa usalama wa Uturuki wamekanusha taarifa kuwa raia wake wawili waliokamatwa na vikosi vya mbabe wa kivita nchini Libya, Jenerali Khalifa Haftar ni majasusi.

Wafanyakazi hao waliokuwa wanafanya kazi kwenye mgahawa mmoja mashariki mwa mji unaokaliwa na wanajeshi wa Haftar, walikamatwa April 12 kwenye wilaya ya Ghashir wakituhumiwa kwa ujasusi.

Katika hatua nyingine kiongozi mmoja wa kundi la wapiganaji waliokuwa wanaiunga mkono Serikali ya Tripoli Meja Jenerali Omar Abdel Jalil ametangaza kumuunga mkono Jenerali Haftar.

Haya yanajiri wakati huu kukiendelea kuripotiwa mapigano makali nje kidogo ya mji wa Tripoli kati ya wanajeshi wa Serikali na wale wa Jenerali Haftar.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana