Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Maambukizi ya Ebola yaongezeka Mashariki mwa DRC

media Wafanyakazi wa kituo cha kutoa matibabo kwa wagonjwa wa Ebola katika Wilaya ya Butembo wanashughulikia mwanamke aliyambukizwa virusi vya Ebola Machi 28, 2019. REUTERS/Baz Ratner

Watu 26 wamethibitishwa kufa ndani ya siku moja kwenye jimbo la Kivu Kaskazini kutokana na maradhi ya ugonjwa wa Ebola unaoendelea, kusumbua nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mlipuko wa sasa ni wa pili mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa baada ya ule uliokumba maeneo ya Afrika Magharibi mwaka 2014-2016 na kuua watu zaidi ya elfu 11.

Wizara ya afya nchini DRC imethibitisha vifo vya watu 957, huku ikirekodi visa vya watu 891 ambao wana maambukizi ya ugonjwa huo.

Serikali imetangaza mikakati zaidi ya kukabiliana na kuenea kwa maambukizi zaidi.

Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola Mashariki mwa DRC yameendelea kuwa magumu kutokana na makundi ya waasi kushambulia vituo vya afya vinavyotoa matibabu kwa wagonjwa wa Ebola.

Kituo kinachotoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa wa Ebola kilichoshambuliwa Katwa, Februari 25, 2019. Laurie Bonnaud/MSF/Handout
Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana