Hata hivyo baadhi ya vyama vya kisiasa viliamua kususia mkutano huo, kufuatia kile vyama hivyo vinasema unaenda kinyume na matakwa ya wananchi.
"Wananchi wa Algeria wanataka mabadiliko halisi. Hawakubaliana kwamba utawala uendelee kuongozwa na watu waliokuwa chini ya uongozi wa utawala wa rais Abdelaziz Bouteflika. Sote tunaomba Bensalah kuondolewa kwenye nafasi hiyo, anapaswa kuondoka. Ni vizuri kusikia wito wa wananchi wa Algeria na kisha tutaketi kwenye meza ya mazungumzo, " amesema Abderrazak MAkri kiongozi wa chama cha MSP.
Maandamano yameendelea kushuhudiwa nchini Algeria ambapo wananchi wameomba kuondolewa kwa mfumo wote wa utawala uliokuwa chini ya rais aliyelazimishwa kujiuzulu, Abdelaziz Bouteflika.