Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Sudani: Waandamanaji waendelea kushinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa raia

media Waandamanaji wameendelea kupiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi, wakitaka jeshi kukabidhi madaraka kwa raia. Photo: AFP

Waandamanaji nchini Sudani wameapa kuendelea na maandamano yao licha ya kuzuiliwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Omar Hassan al-Bashir, hadi pale jeshi litakabidhi madaraka kwa raia.

Ni wiki moja kamili tangu jeshi nchini Sudan lilipomwondoa madarakani rais wa zamani Omar Al Bashir, kutokana na maandamano ya wananchi.

Bashir ambaye alikuwa ameongoza nchi hiyo kwa miaka 30, Jumatano wiki hii, alihamishiwa kwenye Gereza la Kober jijini Khartoum.

Hata hivyo waandamanaji bado wameendelea kupiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi, wakitaka madaraka nchini humo kukabidhiwa kwa raia.

Jeshi limeendelea kupata shinikizo kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Mapema wiki hii Baraza la amani na Usalama la Umoja wa Afrika, linlitaka jeshi nchini Sudan kukabidhi madaraka kwa raia kwa muda wa siku 15 zijazo, au nchi hiyo isimamishwe kuwa mwanachama wa Umoja huo.

Wito huu wa Umoja wa Afrika, umekuja wakati huu waandamanaji wakiendelea kusalia nje ya makao makuu ya jeshi kushinikiza serikali nchini humo kuundwa na raia wa kawaida.

Jumatatu wiki hii Luteni Jenerali Jalal al-Deen al-Sheikh, mmoja wa viongozi wa kijeshi alikutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia jijini Addis-Ababa na kusema kuwa, uongozi wa jeshi upo kwenye mchakato wa kumteua Waziri Mkuu, ambaye ataongoza serikali ya kiraia.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana