Pata taarifa kuu
MISRI-KURA YA MAONI-SIASA

Misri: Kura ya maoni kupigwa kati ya Aprili 20 na 22

Raia wa Misri, kati ya tarehe 20 na 22 mwezi huu, watapigia kura mabadiliko yaliyofanywa na wabunge kumruhusu rais Abdel Fattah al-Sisi kuwa madarakani hadi mwaka 2030.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi. RFI/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Wabunge pia wanataka jeshi la nchi hiyo lipewe nafasi kubwa ya kuamua mustakabali wa hali ya kisiasa kwenye taifa hilo.

Hata hivyo, wadadisi wa siasa wanaonya kuwa huenda mabadiliko hayo yakaitumbukiza nchi hiyo kwenye mzozo mwingine wa kisiasa licha ya kuwa jeshi bado linaungwa mkono.

Mbali na mabadiliko hayo, wabunge wamempa rais Al Sisi mamlaka makubwa ya kudhibiti idara ya Mahakama lakini pia jeshi kuendelea kuwa na usemi mkubwa katika siasa za nchi hiyo ya Afrika ya Kaskazini.

Rais Al Sisi, ambaye alichaguliwa mwaka 2018, muhula wake wa miaka sita ulitarajiwa kumalizika mwaka 2024, lakini iwapo mabadiliko hayo yataungwa mkono, anaweza kuchagulia tena kwa muhula mwingine wa miaka sita.

Al Sisi aliingia madarakani mwaka 2013, baada ya kuongoza mapinduzi ya kijeshi kumpindua rais aliyekuwa amechaguliwa wakati huo Mohamed Morsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.