Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Rais wa zamani wa Sudan ahamishiwa katika jela la mji mkuu

media Aliye kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir (Picha ya zamani). AFP/Ashraf Shazly

Rais wa zamani wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir, aliyepinduliwa madarakani wiki iliyopita, amehamishiwa katika jela la Kobar jijini Khartoum. Omar Hassan al-Bashiri anazuiliwa katika jela la Kobar tangu Jumanne jioni wiki hii, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Kiongozi huyo wa zamani, ambaye alitawala Sudan tangu mwaka 1989, alikuwa mpaka sasa chini ya ulinzi wa kifungo cha nyumbani.

Bashir, ambaye alielemewa na maandamano kwa miezi kadhaa, alishinikizwa kuachia ngazi na jeshi, Aprili 11 mwaka huu.

Jeshi kwa sasa ndilo linashikilia madaraka, licha ya shinikizo kutoka kwa waandamanaji na mataifa kadhaa ikiwa ni pamoja na nchi zeye nguvu duniani kutaka jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.

Mapema wiki hii Baraza la amani na Usalama la Umoja wa Afrika, linlitaka jeshi nchini Sudan kukabidhi madaraka kwa raia kwa muda wa siku 15 zijazo, au nchi hiyo isimamishwe kuwa mwanachama wa Umoja huo.

Wito huu wa Umoja wa Afrika, umekuja wakati huu waandamanaji wakiendelea kusalia nje ya makao makuu ya jeshi kushinikiza serikali nchini humo kuundwa na raia wa kawaida.

Jumatatu wiki hii Luteni Jenerali Jalal al-Deen al-Sheikh, mmoja wa viongozi wa kijeshi alikutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia jijini Addis-Ababa na kusema kuwa, uongozi wa jeshi upo kwenye mchakato wa kumteua Waziri Mkuu, ambaye ataongoza serikali ya kiraia.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana