Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Tshisekedi aahidi amani na usalama Goma

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ameendelea kuzuru jimbo la Kivu Kaskazini na jana alikutana na wakuu wa usalama mjini Goma, huku ziara yake ikiwa ni kuwahakikishia usalama raia wa eneo hilo lakini pia kutathmini mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi awataka raia kuchangia katika kurejesha amani na usalama Mashariki mwa DRC.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi awataka raia kuchangia katika kurejesha amani na usalama Mashariki mwa DRC. Stringer/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa kampeni yake katika uchaguzi wa urais na baada ya kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi alisema atajikita na kurejesha amani na usalama katika maeneo ya mashariki na Kusini magharibi mwa DRC. Siku ya Jumatatu, mbele ya viongozi waliochaguliwa wa moka wa Kivu Kaskazini, rais Felix Tshisekedi alielezea nia yake ya kurejesha usalama na amani katika mkoa huo unaoendelea kukumbwa na utovu wa usalama."

“Sina maajabu yoyote ambayo ninaweza kufanya, nina nia nzuri ya kubadili mambo. Ninawahitaji. Muna uwezo wa ushawishi. Kupitia mazungumzo yenu na mitazamo yenu, mnaweza kuchangia pamoja na mi kurejesha amani, " aliwaambia viongozi waliochaguliwa katika ngazi ya taifa na mkoa ambao wameonya mara kadhaa kuhusu ukosefu mkubwa wa usalama katika mkoa huo.

Rais Felix Tshisekedi Tshilombo aliwasili Jumapili Aprili 14 jijini Goma, mkoa wa Kivu Kaskazini ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kwanza ndani ya nchi tangu kuchaguliwa kwake Mwezi Desemba mwaka jana.

Kabla ya ziara yake hiyo jijini Goma alianza kuzuru mji wa Lubumbashi. Maeneo yate hayo mawili yanaendelea kukumbwa na utovu wa usalama lakini pia maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola katika mkoa wa Kivu kakazini, hasa katika maeneo ya Beni na Butembo.

Baada yakuapishwa kwake kipaombele cha rais Tshisekedi ilikuwa ni ziara za nje kuliko za ndani.

Tangu kuapishwa kwake Januari mwaka huu rais Tshisekedi amesha fanya ziara katika mataifa zaidi ya 5, ikiwa ni pamoja na nchi jirani ya Rwanda na Uganda bila kusahau Kenya ambapo rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais Tshisekedi mjini Kinshasa.

Tangu kuchaguliwa kwake kuwa rais wa DRC, rais Tshisekedi hajatangaza baraza lake la mawaziri.

Hata hivyo kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na ikulu ya Kinshasa serikali mpya inayotarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.