Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA-MAANDAMANO

Sudani: Utawala mpya wajaribu kushawishi waandamanaji

Utawala mpya nchini Sudani unaendelea na operesheni yake wa kuwakamata 'wahalifu' na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono baraza la kijeshi la mpito, ambalo lilimtimua mamlakani rais Omar al-Bashir wiki iliyopita.

Mandamano mbele ya makao makuu ya jeshi, Khartoum,Aprili 14, 2019.
Mandamano mbele ya makao makuu ya jeshi, Khartoum,Aprili 14, 2019. ©AHMED MUSTAFA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Utawala wa kijeshi pia umetoa wito kwa viongozi wa maandamano na upinzani kupendekeza jina la mtu atakaye shikilia nafasi ya waziri mkuu.

Mkuu mpya wa idara ya upelelezi alitangazwa Jumapili usiku nchini Sudan. Jenerali Aboubaker Moustafa anachukuwa nafasi ya mtangulizi wake Salah Gosh ambaye alijiuzulu siku ya Jumamosi.

Mkuu wa idara ya upelelezi nchini Sudani (NISS) ni miongoni mwa watu wanaonyooshewa kidole kwa ukandamizaji dhidi ya waandamanaji na viongozi wa maandamano.

NISS ni mmoja wa wahusika wakuu wa ukandamizaji wa maandamano ya miezi 4 iliyopita.

Tangazo jingine la kufutwa kazi ni lile la afisa wa ubalozi wa sudan jijini Washington, Mohamed Atta, mkuu wa zamani wa idara ya upelelezi.

Wakati huo huo jeshi limeamua kuteua mtu kutoka upinzani ambaye atashikilia nafasi ya waziri mkuu.

Jeshi limeomba viongozi wa maandamano na upinzani kuafikiana kwa jina la mtu mmoja ambaye atashikilia nafasi hiyo.

Waziri Mkuu huyo atakuwa na jukumu la kuunda serikali ya kiraia.

Hatua hiyo imefikiwa katika mkutano kati ya Baraza la kijeshi na vyama vya siasa Jumapili, Aprili 14. Lakini viongozi wa maandamano wamefutilia mbali hoja hiyo na kulitaka jeshi kuachia madaraka kwa raia.

Hata hivyo mkutano huo ulisusiwa na viongozi wa maandamano, "kundi linalotetea uhuru na mabadiliko", muungano ambao unajumuisha vyama vya upinzani na wasomi kutoka sekta mbalimbali nchini Sudani. Walikataa kushiriki mkutano huo kwa sababu ya kuwepo kwa chama cha Omar al-Bashir.

Wawakilishi hawa wa maandamano pia wanasema wanasubiri majibu kutoka Baraza la kijeshi kwa mfululizo wa mapendekezo waliotoa siku ya Jumamosi. Miongoni mwa mapendekezo hayo ni pamoja na kufuta Baraza la kijeshi au kuwashirikisha raia katika baraza hilo, au kukubali kuwa baraza hilo halitakiwi kushikilia mamlaka yote.

Mvutano unaendelea jijini Khartoum ambapo waandamanaji wanaendelea na madai yao, ya kukabidhi haraka serikali kwa raia. Pia wataka Omar Hassan al-Bashir ahukumiwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.