Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Mapigano yaendelea kurindima karibu na Tripoli

Wanajeshi wa serikali ya Libya, inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, wameangusha ndege ya kivita ya mpinzani wa serikali hiyo Jenerali Khalifa Haftar anayeongoza serikali pinzani Mashariki mwa nchi hiyo.

Wapiganaji wa kundi la ANL yanayoongozwa na Marshal Khalifa Hafta, yakiondoka Benghazi na kwenda kuwasadia wenzao wanaoelekea Tripoli, Benghazi, Libya, Aprili 7, 2019.
Wapiganaji wa kundi la ANL yanayoongozwa na Marshal Khalifa Hafta, yakiondoka Benghazi na kwenda kuwasadia wenzao wanaoelekea Tripoli, Benghazi, Libya, Aprili 7, 2019. © REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Kuangushwa kwa ndege hiyo kumekuja wakati Jenerali Khalifa Haftar, akikutana na mshirika wake wa karibu, rais wa Misri Abdel Fatah al Sisi.

Ripoti kutoka Tripoli, zinasema kuwa ndege hiyo iliangushwa Kuisni mwa jiji hilo wakati huu jeshi tiifu kwa serikali, likiendelea kudhibiti serikali hiyo inayotambuliwa kimataifa.

Wanajeshi wa serikali wanasema wanamtafuta rubani wa ndege hiyo, anayeaminiwa alifanikiwa kujiokoa.

Licha ya wito wa jumuiya ya kimataifa kutoka pande zote mbili kuacha mapigano, Shirika la Msalaba Mwekundu limesema wiki iliyopita watu 121 walipoteza maisha na wengine zaidi ya 500 walijeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.