Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Muungano wa vyama vinavyomuunga mkono Kabila washinda uchaguzi wa Magavana

Chama cha Kabila cha PPRD na washirika wake wanaojumuika katika muungao wa kisiasa wa FCC wameshinda kwa mara nyingine uchaguzi wa Magavana na Manaibu Gavana, uchaguzi ambao ulifanyika Jumatano Aprili 10, 2019 katika mikoa 22 kati ya 26 inayounda DRC.

Felix Tshisekedi atalazimika kuunda serikali yenye Magavana wengi kutoka kambi ya mtangulizi wake.
Felix Tshisekedi atalazimika kuunda serikali yenye Magavana wengi kutoka kambi ya mtangulizi wake. © REUTERS/ Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Chama cha UDPS cha rais Felix Tshisekedi kimepata Gavana mmoja pekee katika mkoa wa Kasai Oriental, pamoja na muungano wa vyama vya upinzani wa Lamuka.

Katika mikoa minne (Haut-Lomami, Kasaï ya Kati, Nord-Ubangui na Tshopo), duru ya pili ya uchaguzi itafanyika Jumamosi wiki hii.

Uchaguzi huu ni pigo kubwa kwa rais wa sasa wa DRC Felix Tshisekedi, ambaye muungano wake wa CASH una viti vichache katika baraza la Wawakilishi, Bunge la Seneti na katika Baraza la Wawakilishi katika ngazi za mikoa.

Kwa hiyo Felix Tshisekedi atalazimika kuunda serikali yenye Magavana wengi kutoka kambi ya mtangulizi wake.

Ndugu ya aliyekuwa rais wa DRC Joseph Kabila, Zoe Kabila, ambaye sasa ni gavana wa Tanganyika, ni miongoni mwa waliochaguliwa.

Naye Christophe Nangaa, ndugu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (CENI) Corneille Nangaa, amechaguliwa kuwa Gavana wa mkoa wa Haut-Uélé dhidi ya mgombea wa FCC.

Wabunge katika ngazi za mikoa ndio walichagua Magavana wa mikoa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.