Pata taarifa kuu
SUDAN-JESHI-MAANDAMANO-BASHIR-SIASA

Jeshi latangaza kuchukua madaraka nchini Sudan, Bashir akamatwa

Jeshi nchini Sudan limetangaza kuchukua uongozi wa nchi hiyo kwa kipindi cha mpito cha miaka miwili baada ya kumwondoa madarakani na kumkamata rais wa zamani Omar Al Bashir.

Kiongozi wa kijeshi nchini Sudan  Awad Mohamed Ahmed Ibn Auf akitangaza hatua ya kuchukua serikali Aprili 11 2019
Kiongozi wa kijeshi nchini Sudan Awad Mohamed Ahmed Ibn Auf akitangaza hatua ya kuchukua serikali Aprili 11 2019 Sudan TV/ReutersTV via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili limekuja baada ya maandamano ya wananchi ambayo yamekuwa yakiendelea tangu mwezi Desemba mwaka 2018, kushinikiza kujiuzulu kwa rais Bashir baada ya kupanda kwa bei ya mafuta na mkate.

Akitoa tangazo hilo, Waziri wa Ulinzi Awad Ibnouf amesema, jeshi litaongoza kwa kipindi cha mpito, kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi mpya na kupatikana kwa katiba mpya.

“Natangaza kama Waziri wa Ulinzi, kuondolewa madarakani kwa uongozi uliokuwepo na kukamatwa kwa kiongozi wake,” ametangaza kupitia Televisheni ya taifa siku ya Alhamisi mchana.

Aidha, Ibnouf ameeleza kuwa mbali na hatua hiyo, hali ya hatari itashuhudiwa nchini humo kwa muda wa miezi mitatu kati ya saa nne usiku hadi saa 10 Alfajiri.

Wafungwa wote wa kisiasa wanatarajiwa pia kuachiliwa huru, baada ya tangazo hili.

Licha ya tangazo hili, waandamanaji wameonekana kutoridhishwa na maelezo ya jeshi, kwa kile wanachosema kuwa wanataka raia kuongoza serikali hiyo ya mpito.

Bashir ameondolewa madarakani, baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 20, baada ya mapinduzi ya kijeshi ambayo hayakushuhudia umwagaji damu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.