Pata taarifa kuu
LIBYA-UN-MAPIGANO-USALAMA

Umoja wa Mataifa waahirisha mkutano kati ya Walibya

Mkutano kati ya Walibya uliokuwa unatarajiwa kufanyika hivi karibuni kati ya wadau wote katika mgogoro wa Libya umeahirishwa na Umoja wa Mataifa.

Wapiganaji wa kundi la ANL yanayoongozwa na Marshal Khalifa Hafta, yakiondoka Benghazi na kuam kuwasadia wenzao wanaoelekea Tripoli, Benghazi, Libya, Aprili 7, 2019.
Wapiganaji wa kundi la ANL yanayoongozwa na Marshal Khalifa Hafta, yakiondoka Benghazi na kuam kuwasadia wenzao wanaoelekea Tripoli, Benghazi, Libya, Aprili 7, 2019. REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo ulitarajia kusaidia nchi hiyo kuondokana na mgogoro, lakini mapigano yanayoendelea karibu na mji mkuu wa Libya, Tripoli, kati ya pande hasimu yamesababisa uahirishwe.

"Hatuwezi kuomba Walibya kushiriki katika mkutano, wakati wanaendelea kupigana wenyewe kwa wenyewe, mashambulizi ya angani yanaendelea kutekelezwa," mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Ghassan Salame, amesema katika taarifa.

Bw Salame anatarajia kuelezea uamuzi wake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo linatarajia kukutana leo Jumatano kwa kikao cha dharura na cha faragha, wanadiplomasia wamesema mjini New York.

Makabiliano kati ya wanajeshi wa serikali wanaotambuliwa na Jumuiya uya Kimataifa na wale wa Jenerali Khalifa Haftar kwa karibu wiki moja sasa, yamesababisha maelfu ya watu kuyakimbia makwao.

Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya haki za binadamu inaonya kuwa mauaji ya raia 47 ndani ya siku tatu, yanaelekea kuwa uhalifu dhidi ya binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.