Pata taarifa kuu
ALGERIA-SIASA-VYOMBO VYA HABARI

Mkurugenzi wa AFP Algiers afukuzwa

Mkurugenzi wa shirika la Habari la AFP nchini Algeria, Aymeric Vincenot, amefukuzwa na mamlaka nchini humo, ambayo imekataa kuongeza muda wa kibali chake kinachomruhusu kuishi nchini Algeria kwa mwaka huu 2019.

Vincenot Aymeric, mkurugenzi wa shirika la Habari la AFP nchini Algeria, Machi 1, 2019, Algiers.
Vincenot Aymeric, mkurugenzi wa shirika la Habari la AFP nchini Algeria, Machi 1, 2019, Algiers. © AFP
Matangazo ya kibiashara

atua hiyo inakuja wakati Algeria inaendelea kukumbwa na maandamano makubwa ambayo yalimshinikiza rais Abdelaziz Bouteflika kuachia ngazi, baada ya kujaribu ktangaza kwamba atawania katika uchaguzi wa urais kwa muhula wa tano, na kisha kujiuzulu tarehe 2 Aprili.

Maandamano hayo ya amani ambayo yalianzishwa Februari 22, yakiongozwa na vijana, yanaendelea. Kwa sasa wandamanaji wanataka mfumo wote unaotawala Algeria tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake mnamo mwaka 1962 uondolewe.

Bw Vincenot, mwenye umri wa miaka 45, ambaye alikuwa akiishi Algeria tangu mwezi Juni 2017, aliondoka Algeria Jumanne usiku baada ya muda wake wa mwisho kuishi nchini humo kumalizika jana.

"Uamuzi uliochukuliwa chini ya utawala wa Abdelaziz Bouteflika haukubaliki. Katika mazingira haya, hatuwezi kuteua kwa wakati huu mkurugenzi mpya nchini Algeria," Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Habari la AFP, Fabrice Fries, amesema katika taarifa.

Hata hivyo Bw Fries amesema, licha ya uamuzi huo, shirika lake litaendelea kuhabarisha umma kwa yale yanayotokea nchini Algeria, na litaendelea na mchakato wa kutafuta visa kwa wanahabari wake wengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.