Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Algeria: Abdelkader Bensalah ahadi 'uchaguzi wa urais' ulio wazi

Katika hotuba iliyorushwa kwenye televisheni Jumanne jioni, Abdelkader Bensalah, ambaye kwa sasa ni kaimu rais wa Algeria, ametangaza kuwa uchaguzi utafanyika ndani ya siku 90 na kwamba tume itakayoandaa uchaguzi huo itakuwa imeteuliwa.

Abdelkader Bensalah baada ya kuteuliwa na Bunge la Algeria Aprili 9, 2019.
Abdelkader Bensalah baada ya kuteuliwa na Bunge la Algeria Aprili 9, 2019. © REUTERS/Ramzi Boudina
Matangazo ya kibiashara

Abdelkader Bensalah, ambaye ameteuliwa na Bunge kukaimu nafasi ya rais, ameahidi Jumanne usiku kuwa ataandaa "uchaguzi wa urais huru na ulio wazi " ndani ya siku 90.

Mimi, rais wa Baraza la Wawakilishi, nachukua nafasi ya rais kwa muda wa siku 90. Katika kipindi hiki, ninajikubalisha leo mbele yenu kuandaa uchaguzi wa urais, amesema Abdelkader Bensalah.

Spika wa Bunge hatimaye amekuwa kaimu rais. Kwa hivyo, mamlaka yake yamepunguzwa. Moja ya kazi yake kubwa ni kuandaa uchaguzi wa urais. Kwa hiyo ana muda wa siku 90, kuitisha wananchi wa Algeria kupiga kura, kumchagua rais wao mpya. Bila shaka, hana haki ya kuwania katika uchaguzi huo.

Kwa sasa, serikali ya Algeria na Bunge vitaendelea kufanya kazi. Kaimu rais hana haki ya kuunda serikali mpya au kufuta Bunge. Kwa hiyo atahitaji pia ridhaa ya wabunge na maseneta kwa kikao maalumu cha Bunge, ikiwa anataka kutangaza hali ya dharura, kwa mfano.

Hakuna suala la kufanya marekebisho yoyote kwenye Katiba. Hakuna marekebisho yoyote yanayoweza kufanywa wakati wa kipindi hiki cha miezi mitatu. Abdelkader Bensalah hawezi kutoa msamaha kwa wafungwa au kuitisha kura ya maoni.

Wakati huo huo waandamanaji wanaendelea kumiminika mitaani wakitaka Bensalah ajiuzulu, wakimtuhumu kuwa ni miongoni mwa kundi linaloongoza Algeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.