Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA-MAANDAMANO

Waandamanaji waomba mazungumzo na jeshi Sudan

Waandamanaji wanaendelea kuandamana kwa siku ya tatau mfululizo karibu na makao makuu ya jeshi la Sudan katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.

Maandamano yanayomtaka rais al-Bashir kujiuzulu, Khartoum, Aprili 6, 2019.
Maandamano yanayomtaka rais al-Bashir kujiuzulu, Khartoum, Aprili 6, 2019. © REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu wiki hii waandamanaji hao wameomba mazungumzo ya moja kwa moja na jeshi kwa ajili ya kuundwa serikali ya mpito itakayochukua nafasi ya rais Omar al-Bashir. Msimamo wa hivi karibuni wa jeshi unaonekana kuwapa nguvu.

Katika taarifa iliyosomwa mbele ya watu zaidi ya 40,000 waliokusanyika, tangu Jumamosi mbele ya makao makuu ya jeshi katikati mwa jiji la Khartoum, ujumbe wa upinzani ulitowa wito wake wa kumtaka rais ais al-Bashir na serikali yake wajiuzulu. Taarifa hiyo inaomba kuundwa kwa Baraza Kuu, litakalo wajumuisha wawakilishi wa jeshi na waandamanaji ili kujadili utaratibu wa kuondoka rais wa nchi hiyo na pia kuundwa kwa serikali ya mpito.

Hayo yanajiri wakati vikosi vya usalama vimezingira tangu mapema Jumanne Alfajiri maeneo kadhaa katika mji mkuu wa Sudan ili ku kakabiliana na watu wanaoendelea kuelekea karibu na makao makuu ya jeshi ambapo wamekusanyika waandamanaji.

Jumatatu Aprili 8 kulitokea makabiliano kati ya jeshi na vikosi vya usalama wakati baadhi ya maafisa wa polisi walijaribu kurusha risasi hewani na mabomu ya kutoa machozi kwa lengo la kuwatawanya waandamanaji.

Kw mujibu wa mwandishi wa habari Chawgui Abdel Azim ambaye alihojiwa na RFI, kumekuwa na hali ya sintofahamu katika jeshi na kwamba vitengo kadhaa vya jeshi vimeasi amri ya Waziri. Ametoa ushuhuda juu ya ushirikiano huu wa baadhi ya askari na waandamanaji.

"Magari ya jeshi sasa yanazuia njia zote zinazoelekea eneo ambapo waandamanaji wamekusanyika. Waandamanaji sasa wanapewa ulinzi na jeshi. Vikosi vya usalama na wanamgambo wanaotoa msaada kwa vikosi hivyo hawawezi kuthubutu tena kuwatawanya", amesema Abdel Azim.

Jumatatu jioni Waziri wa Ulinziu alibaini kwamba "vikosi vya jeshi vinaelewa sababu za maandamano na havipingi malalamiko au madai ya wananchi, lakini havitokubali nchi itumbukie katika machafuko".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.