Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aomba mapigano kusitishwa haraka Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mapigano yanayoendelea karibu na mji mkuu wa Libya, Tripoli, na kuzitaka pande husika kusitisha haraka mapigano.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres na Marshal Khalifa Haftar walikutana Benghazi Aprili 5, 2019.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres na Marshal Khalifa Haftar walikutana Benghazi Aprili 5, 2019. Media office of the Libyan Army/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Bw Guterres amekumbusha kwamba hakuna ufumbuzi wa kijeshi katika mgogoro nchini Libya na amezitaka pande zote "kushiriki mara moja katika mazungumzo ili kupata suluhisho la kisiasa," amesema katika taarifa Stephane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Uwanja wa ndege pekee ambao umekuwa ukifanya kazi jijini Tripoli ulishambuliwa na ndege za kivita za vikosi vya Marshal Khalifa Haftar, ambavyo vinaendesha mashambulizi mabaya dhidi ya mji mkuu wa Libya.

Tangu Alhamisi, vikosi vya Marshal Khalifa Haftar (ANL) vinavyodhibiti mashariki mwa Libya vinapigana na majeshi ya serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, na kusababisha watu wengi kupoteza maisha na zaidi ya 3,400 kuyatoroka makaazi yao

Majeshi ya ANL yamekiri kuwa ndege zao ziliendesha mashambulizi dhidi ya uwanja wa ndege wa Mitiga, mashariki ya Tripoli, na kusababisha kusitishwa kwa safari za ndege na abiria pamoja na wafanyakazi kuondolewa, hata kama mashambulizi hayo hayakusababisha vifo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.