Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-SIASA

Askari wa Sudan walinda waandamanaji Khartoum

Askari wa Sudan wametoa ulinzi kwa maelfu ya waandamanaji wanaopinga serikali, ambao vikosi vya usalama vimekuwa vinajaribu kuwatawanya katikati mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum, mashahidi na waandamanaji wamesema.

Waandamanaji katika makao makuu ya jeshi, Khartoum, Sudani.
Waandamanaji katika makao makuu ya jeshi, Khartoum, Sudani. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Askari hao wameingilia kati ili kulinda waandamanaji waliokuwa wamekuja kuandamana usiku wa pili mbele ya Wizara ya Ulinzi, katikati mwa mji Khartoum, ambapo vikosi vya usalama vilipewa majukumu ya kukabiliana na waandamanaji katika mji huo.

Maandamano ya wapinzani wa rais Omar al Bashir yanafanyika mbele ya Wizara ya Ulinzi, karibu na makao makuu ya ofisi ya rais.

Tangu mwezi Desemba mwaka jana, Sudan imeendelea kukumbwa na maandamano dhidi ya utawala wa rais Bashir, ambaye yuko madarakani tangu mwaka 1989.

Waandamanaji kadhaa wameuawa na vikosi vya usalama vilitumia gesi ya machozi, gruneti hata risasi dhidi ya waandamanaji, lakini rais Bashir amepinga kujiuzulu, mashahidi wamesema.

Mtu mmoja aliuawa Jumamosi wakati wa "maandamano" huko Omdurman, mji ulio karibu na Khartoum, shirika la habari la habari la Suna liliripoti, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu mazingira ya kifo chake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.