Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-BASHIR-SIASA

Maelfu waandamana mbele ya makao makuu ya jeshi nchini Sudan

Maelfu ya waandamanaji nchini Sudan kwa mara ya kwanza waliandamana hadi katika makao makuu ya jeshi jijini Khartoum siku ya Jumamoso, wakiendelea kushinikiza kujiuzulu kwa rais Omar Al Bashir.

Waandamanaji jijini Khartoum nchini Sudan
Waandamanaji jijini Khartoum nchini Sudan Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wakiwa na mabango na kuimba jeshi moja na, watu wamoja, maandamano hayo yaliendelea licha ya serikali kutangaza hali ya hatari nchini humo.

Waandamanaji wanasema, lengo la kufka katika makao makuu ya jeshi ni kutuma ujumbe  mzito kwa wanajeshi kuamua iwapo wanasimama na wananchi au hapana.

“Bado hatujatimiza lengo letu, lakini ujumbe wetu umefikia uongozi wa jeshi,” mmoja wa waandamanaji Amir Omer ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa, AFP.

“Tunamtaka rais Bashir ajiuzulu,” mwingine alisema.

Maandamano hayo pia yalifanyika katika mji mwingine wa Omdurman na kusababisha mwandamanaji mmoja kupoteza maisha.

Bashir mwenye umri wa miaka 75, amekuwa akiongoza nchi hiyo kwa miaka 26.

Hivi karibuni, alinukuliwa akisema anaelewa baadhi ya malalamishi ya waandamanaji hasa suala la ukosefu wa ajira kwa vijana, na kuahidi kuja na mpango wa kutekeleza hilo.

Hata hivyo, anawashatumu wapinzani wa kisiasa kwa kuchochea maandamano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.