Pata taarifa kuu
DRC-MAREKANI-USHIRIKIANO

DRC: Rais Felix Tshisekedi azuru Marekani

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi Tshilombo yuko ziarani tangu Jumatano wiki hii jijini Washington, nchini Marekani, kwa ziara ya siku mbili hadi Aprili 5.

Rais wa DRC pamoja na Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo Washington, Aprili 3, 2019.
Rais wa DRC pamoja na Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo Washington, Aprili 3, 2019. © ANDREW CABALLERO-REYNOLDS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Felix Tshisekedi amechagua Marekani kwa ziara yake rasmi ya kwanza nje ya bara la Afrika tangu alipochukuwa hatamu ya uongozi wa nchi.

Kwa mujibu wa mtafiti Jason Stearns, Marekani, "haikuonesha msimamo wake" kuhusiana na kuchaguliwa kwake kama rais wa DRC wakati nchi nyingine za Magharibi "zilionesha msimamo wao wa kutokuwa na imani na matokeo ya uchaguzi".

Hata hivyo, hakutakuwa na mkutano kati ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Donald Trump. Lakini, kwa mujibu wa Jason Stearns, "hakuna haja ya kutafsiri hali hiyo kama pigo kwa Felix Tshisekedi".

Tshisekedi anakutana na Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo, pia anatarajia kukutana na Seneta Cory Booker; na kutakuwa na mikutano mingi yenye lengo kubwa kuhusu uwekezaji katika sekta ya kibinafsi.

Hata hivyo kwa mujibu wa mtafiti, Felix Tshisekedi anajua kwamba Marekani inaweza kuwa mshirika wake mkubwa dhidi ya mtangulizi wake Joseph Kabila, lakini uungwaji huu mkono wa Marekani sio masharti. Uungwaji mkono wa Marekani kwa utawala wa Tshisekedi unaendana na matarajio yao.

Lengo la Marekani ni kujaribu kuunga mkono Tshisekedi kwa njia nzuri na wakati huo huo kuweka shinikizo kwa serikali ya zamani ya Joseph Kabila, amesema Jason Stearns.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.