Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 07/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 08/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Ethiopia kutoa ripoti kuhusu ajali ya Boeing 737 MAX

media Ndege hiyo yenye chapa 302 iliyokuwa ikisafiri kutoka Addis Ababa kwenda Nairobi ilianguka kwenye shamba, karibu na mji mkuu wa Ethiopia, dakika sita tu baada ya kuruka na kuua watu 157. REUTERS/Tiksa Negeri

Ethiopia imesema kuwa haitatoa Jumatatu wiki hii ripoti ya awali kuhusu sababu za ajali ya ndege aina ya Boeing 737 MAX ya shirika la ndege la Ethiopian Airlines, ambayo iliua watu 157 Machi 10, lakini inaweza kutoa ripoti hiyo baadaye wiki hii, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia.

"Sio leo, labda wiki hii," chanzo hicho kimesema kuhusu kutolewa kwa ripoti hiyo, na kukanusha taarifa za awali zilizotolewa na msemaji wa serikali.

Ndege hiyo yenye chapa 302 iliyokuwa ikisafiri kutoka Addis Ababa kwenda Nairobi ilianguka kwenye shamba, karibu na mji mkuu wa Ethiopia, dakika sita tu baada ya kuruka. Abiria kutoka mataifa zaidi ya 30 walikuwa kwenye ndege hiyo waliangamia.

Ajali hiyo ilitokea miezi mitano baada ya ajali nyingine pia iliyohusisha Boeing 737 MAX 8. Ndege hiyo ya shirika la ndege la Indonesia la Lion Air ilianguka mnamo mwezi Oktoba mwaka jana na kuua watu 189.

Ajali ya Boeing 737 MAX ya Shirika la ndege la Ethiopian Airlines ilisababisha ndege za aina hiyo kupigwa marufuku kusafiri katika nchi mbalimbali duniani.

Uchunguzi kuhusu ajali ya ndege hiyo unaenelea.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana