Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Maandamano yaendelea Algeria

Algeria inatarajiwa kukumbwa na maandamano makubwa Ijumaa hii Machi 29. Wananchi wa Algeria wanaotaka mabadiliko ya utawala wanatarajia kumiminika mitaani kwa Ijumaa ya kwanza ya maandamano baada ya rais Abdelaziz Bouteflika kutengwa na jeshi. 

Raia wa Algeria waishio nchini Ufaransa wakiunga mkono maandamano ya ndugu zao nchini Algeria, Paris Machi 17.
Raia wa Algeria waishio nchini Ufaransa wakiunga mkono maandamano ya ndugu zao nchini Algeria, Paris Machi 17. Geoffroy VAN DER HASSELT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wadadisi wanasema hatua ya jeshi kumtenga Bouteflika ni katika lengo la kuzuia maandamno yanayoendelea kwa miezi kadhaa nchini humo.

Mapema wiki hii Mkuu wa majeshi ya Algeria kwa miaka 15, Jenerali Ahmed Gaid Salah, ambaye ni mshirika wa karibu wa rais Bouteflika aliomba Mahakama ya Katiba kutekeleza Ibara ya 102 inayoonyesha kuwa rais huyo ameshindwa kutekeleza majukumu yake kutokana na kudhoofika kwa afya yake.

Wale ambao, kwa miezi kadhaa, wamemuunga mkono Bouteflika kuwania uchaguzi wa urais ujao kwa muhula wa tano wameanza kujitenga na rais huyo.

Siku ya Alhamisi, Ali Haddad alitangaza kujiuzulu kutoka shirikisho la wakuu wa makampuni (FCE), shirikisho la waajiri wa Algeria, ambalo amekuwa anaongoza. Shirikisho hilo lilikuwa chombo cha msaada wa kisiasa kwa Abdelaziz Boteflika na liliunga mkono kuwania kwake kwa muhula watano katika uchaguzi ujao.

Kabla yake, chama cha National Democratic Rally (RND), chama kinachoshirikiana na chama tawala nchini Algeria kuongoza serikali, kiliunga mkono kauli ya jeshi, kumtaka rais Abdelaziz Bouteflika, kujiuzulu kutokana na kutokuwa na uwezo kuendelea kuongoza kwa sababu za kiafya.

Kiongozi wa chama hicho ambaye ni mshirika wa karibu wa rais Bouteflika, amesema kiongozi huyo ameihudumia nchi kwa muda mrefu na ni wakati wa kuondoka.

Maandamano yameendelea kushuhudiwa nchini Algeria licha ya rais Bouteflika, mwenye umri wa miaka 82 kuendelea kusalia madarakani, licha ya kutangaza kuwa hatawania tena urais.

Kwa upande mwengine mwenyekiti wa taasisi ya vijana nchini Algeria, Addad Hakim amesema wao wataendelea na maandamano kwa juma zima kushinikiza kuondoka madarakani kwa wa rais Bouteflika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.