Pata taarifa kuu
MALI-MAUAJI-USALAMA

Idadi ya waliouawa kutoka jamii ya Fulani yaongezeka

Idadi ya vifo vya watu waliouawa kutoka jamii ya Fulani nchini Mali Jumamosi, imeongezeka na kufikia 157, msemaji wa serikali ya Mali ametangaza, huku akibani kwamba shambulio hilo ni baya katika historia ya hivi karibuni ya nchi hiyo.

Watu kutoka jamii ya Fulani wakiandamana kupinga  vitendo viovu wanavyofanyiwa kwa siku kadhaa katikati mwa Mali. Maandamano yalioandaliwa na vijana wa Tabil Pulaaku-Mali, MAchi 15, 2018.
Watu kutoka jamii ya Fulani wakiandamana kupinga vitendo viovu wanavyofanyiwa kwa siku kadhaa katikati mwa Mali. Maandamano yalioandaliwa na vijana wa Tabil Pulaaku-Mali, MAchi 15, 2018. © ANNIE ROSEMBERG / AFP
Matangazo ya kibiashara

Awali serikali ilitangaza kwamba watu 135 kutoka jamii ya Fulani waliuawa katika shambulio hilo.

Mali imeendelea kukabiliwa na machafuko ya kikabila.

Kundi la watu wenye silaha walivamia kijiji kimoja ambacho kinaishi watu kutoka jamii ya Fulani na kuanza kutekeleza kitendo chao kiovu. Katika shambulio watu waliuawa na nyumba kadhaa zilichomwa moto.

Baada ya mauaji hayo rais Ibarahim Boubacar Keita alichukua uamuzi wa kuwaondoa kwenye nafasi zao wakuu kadhaa wa jeshi.

Wakati huo huo serikali ilitangaza kuvunja kundi la wanamgambo la Dan Nan Ambassagou

Mauaji hayo yalitokea katikati mwa nchi ya Mali, karibu na mpaka na Burkina Faso.

Mauaji hayo yalitokea wakati ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikuwa likizuru Mali kujaribu kutafuta ufumbuzi wa machafuko yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.