Pata taarifa kuu
ALGERIA-JESHI-MAANDAMANO-SIASA

Jeshi la Algeria laomba rais Bouteflika kupumzishwa

Mkuu wa jeshi la Algeria, Ahmed Gaed Salah, ameomba rais Bouteflika atangazwe kuwa hana uwezo kiafya kuendelea kushikilia madaraka, kwa mujibu wa kituo cha televisheni Ennahar.

Wananchi wa Algeria waandamana katika mitaa ya mji mkuu Machi 22, 2019, mwezi mmoja baada ya kuzuka kwa maandamano hayo.
Wananchi wa Algeria waandamana katika mitaa ya mji mkuu Machi 22, 2019, mwezi mmoja baada ya kuzuka kwa maandamano hayo. REUTERS/Ramzi Boudina
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo inakuja baada ya mwezi mmoja wa maandamano ya kila siku nchini Algeria, ambapo waandamanaji wanaomba rais Abdelaziz Bouteflika kuachia ngazi.

Mkuu wa jeshi ameongeza kuwa madai ya waandamanaji yanaeleweka na ni halali.

Rais wa Halmashauri ya Taifa, taasisi ya juu ya Bunge la Algeria, Abdelkader Bensalah, atachukua nafasi ya mkuu wa nchi kwa siku 45, kwa mujibu wa wa Katiba, kituo cha televisheni cha Ennahar kimeongeza.

Mkuu wa jeshi nchini Algeria ameomba utekelezaji wa Ibara ya 102 ya Katiba, ambayo haimruhusu rais kuendelea kushikilia madaraka ikiwa atakuwa amedhoofika kiafya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.