Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-SIASA-MAUAJI-UGAIDI

Human Rights Watch yasema, watu 115 wameuliwa na maafisa wa usalama nchini Burkina Faso

Ripoti ya Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch inasema, maafisa wa usalama nchini Burkina Faso wamewauwa kwa kuwanyonga raia wa kawaida 115 tangu katikati ya mwaka 2018.

Wanajeshi wa Burkina Faso
Wanajeshi wa Burkina Faso African Stand
Matangazo ya kibiashara

Imeelezwa kuwa, mauaji haya yalitokea wakati wa operesheni dhidi ya makundi ya kijihadi nchini humo ambayo yamesababisha ukosefu wa usalama.

Serikali ya Burkina Faso haijazungumzia ripoti hii lakini, imekuwa ikikanuisha ripoti kama hizi katika siku zilizopita na kutetea maafisa wake wa usalama, kwa kufanya kazi kubwa ya kupambana na ugaidi.

Mauaji hayo yote yanaelezwa, yalitokea Kaskazini mwa nchi hiyo karibu na nchi ya Mali na Niger kati ya Aprili 2018 hadi Januari 2019.

Corinne Dufka Mkuu wa Human Rights Watch kwenye ukanda wa Sahel amesema, kuwa mauaji hayo yamesababisha raia wengi kuendelea kuishi kwa wasiwasi.

Burkina Faso imetangaza hali ya hatari katika majimbo kadhaa kutokana na vita dhidi ya ugaidi kwa usaidizi wa mataifa ya Magharabi hasa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.