Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-ZIMBABWE-MAJANGA YA ASILI

Idadi yawaliopoteza maisha kufuatia kimbunga Idai yaongezeka

Takwimu za hivi karibuni zinaeleza kuwa watu 300 ndio wamehesabiwa kupoteza maisha kufuatia kimbunga Idai kilichopiga eneo la ukanda wa Afrika Kusini wakati huu mchakato wa kuwaokoa watu waliokimbilia juu ya miti na juu ya paa za majumba.

Picha ya mji wa Beira iliyopigwa mnamo Machi 18 baada ya kimbunga kupiga nchini Msumbiji.
Picha ya mji wa Beira iliyopigwa mnamo Machi 18 baada ya kimbunga kupiga nchini Msumbiji. © IFRC
Matangazo ya kibiashara

Nchini Msumbuji, nchi ilioguswa zaidi na kimbunga hicho, inaelezwa kuwa mpaka sasa ni watu 200 ndio waliopoteza maisha, kulingana na taarifa ya rais wa nchi hiyo Filipe Nyusi ambae ametangaza maombolezo ya siku tatu.

Nchini Zimbabwe zaidi ya watu 100 ndio wanaodaiwa kupoteza maisha, lakini kwa mujibu wa waziri wa serikali za mikoa July Moyo idadi hiyo inaweza kuongezeka mara tatu kwani kuna miili ya watu inayoelea juu ya maji kuelekea nchini Msumbiji.

Wito wa misaada ya kimataifa umetolewa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waliokimbia kutokana na mafuriko hayoyatokanayo na kimbunga Idai. Debora Guyene ni mkurugenzi kwenye shirika la msaada wa chakula la Umoja wa Mataifa PAM.

Upande wake, Serikali ya Tanzania imetowa msaada wa chakula na dawa kwa ajili ya wananchi wamataifa hayo yalioathirika na kumbunga hicho. Kama anavyoelea hapa waziri wa mambo ya nnje wa Tanzania Paramagamba Kabudi

Tayari shughuli za mazishi zimeanza nchini Zimbabwe ambapo rais wa nchi hiyo Emerson Mnangagwa anatarajiwa kuwasili katika eneo la Manikalan eneo lililoguswa zaidi na kimbunga hicho wakati huu shirika la kimataifa la haki za binadamu Amnesty international likitoa wito kwa jumuiya kimataifa kuhamasisha utoaji msaada ili kukabiliana na hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.