Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Tshisekedi azuia zoezi la kuapishwa maseneta wapya

media Rais wa DRC Félix Tshisekedi katika mkutano na waandishi wa habari jijini Luanda, Angola, Februari 5, 2019. Stringer/AFP

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Thisekedi, amesitisha zoezi la kuwaapisha Maseneta wapya waliochaguliwa wiki iliyopita na kuagiza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu madai kuwa, uchaguzi huo uligubikwa na visa vya rushwa.

Pamoja na hili, Uchaguzi wa Magavana uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu, umeahirishwa kwa muda usiojulikana.

Hatua hii imekuja, baada ya muungano wa kisiasa wa rais wa zamani Joseph Kabila, kushinda karibu viti vyote vya Useneta huku muungano wa rais Thisekedi ukilalamikia matokeo hayo.

Rais Felix Tshisekedi ameahidi kukutana na tume ya uchaguzi na maafisa wengine mwanzoni mwa wiki ijayo,

Duru za kuaminika zinabaini kwamba Tshisekedi pia amemtaka mwendesha mashitaka wa serikali kufungua uchunguzi dhidi ya viongozi hao.

Awali Tume ya Uchaguzi nchini DRC (CENI) ilikataa ombi kutoka kwa mwanasheria mkuu wa serikali kusimamisha zoezi la upigaji kura ili kuruhusu polisi kufanya uchunguzi juu ya madai hayo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana