Pata taarifa kuu
DRC-SANA-HAKI

Mwanamuziki nguli DRC Koffi Olomidé ahukumiwa jela miaka miwili

Mahakama ya Uhalifu ya mjini Nanterre nchini Ufaransa imemhukumu jela miaka miwili Mwanamuziki nguli wa Miondoko ya Rumba wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC K Koffi Olomidé baada ya kukutwa na hatia ya makosa ya unyanyasaji wa kingono.

Mahakama ya Nanterre (picha ya kumbukumbu).
Mahakama ya Nanterre (picha ya kumbukumbu). © JACK GUEZ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Olomide alikua anatuhumiwa kwa kumnyanyasa kimapenzi binti wa miaka 15 na wanamuziki wake kati ya mwaka 2002 na 2006 nchini DRC na Ufaransa.

Wanamuziki wake wanne waliokuwa wakimfanyia kazi wameiambia mahakama kwamba aliwanyanyasa kingono mara kadhaa kati ya mwaka 2002 na mwaka 2006.

Olomidé, mwenye umri wa miaka 62, aliagizwa alipe Euro 5,000 kwa madhara aliyomsababishia wanamuziki wake hao wa zamani.

Mahakama pia imemuagiza alipe faini ya kiwango sawa kwa kuwasaidia wanawake wengine watatu kuingia nchini Ufaransa kwa njia haramu.

Mwanasheria wake,Emmanuel Marsinni, amebaini kwamba hukumu iliyotolewa ni ushindi kwa mteja wake kulingana na ukubwa wa kosa la mtuhumiwa.

Awali mwendesha mashitaka aliomba Koffi Olomidé afungwe jela miaka zaidi ya 15.

Hata hivyo hukumu hiyo imeahirishwa mpaka hapo rufaa ya Koffi Olomide itakaposikilizwa baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.