Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-ZIMBABWE-MAJANGA YA ASILI

Kimbunga Idai chaua watu zaidi ya alfu moja Msumbiji

Watu zaidi ya 1, 000 wanahofiwa kupoteza maisha kutokana na kimbuga Idai kilichoshuhudiwa wiki iliyopita nchini Msumbuji na kuathiri mataifa jirani ya Zimbabwe na Malawi.

Baada ya kimbunga Idai kupiga katika baadhi ya maeneo Msumbiji, Machi 18, 2018.
Baada ya kimbunga Idai kupiga katika baadhi ya maeneo Msumbiji, Machi 18, 2018. © AFP PHOTO / MISSION AVIATION FELLOWSHIP / RICK EMENAKET
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa watu wengine zaidi ya 200 hawajapatikana nchini Zimbabwe, suala ambalo limeendelea kuzua wasiwasi mkubwa.

Miili ya watu walipoteza maisha imeonekana, ikielema juu ya maji huku mito kadhaa ikivunja kingo zake katika janga ambalo halijawahi kushuhudiwa nchini Msumbiji.

Mji wa Beira nchini Msumbuji, umeharibiwa kutokana na upepo mkali na mafuruko, na kushuhudia kuporomoka kwa majengo na kuharibika kwa barabara, miongoni mwa miundombinu nyingine.

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amesema watu zaidi ya 100,000 wapo katika hali ya hatari na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.