Pata taarifa kuu
ETHIOUPIA-AJALI-UCHUNGUZI

Ethiopia: Ajali ya Boeing 737 Max 8 yafananishwa na ile iliyotokea Indonesia

Waziri wa Uchukuzi nchini Ethiopia Dagmawit Moges amesema mazingira yaliyosababisha kuanguka kwa ndege ya abiria Boeing 737 Max 8 wiki mbili zilizopita na kusababisha vifo vya watu wote 157, ni sawa na yale yaliyosababisha ndege kama hiyo nchini Indonesia mwaka uliopita.

Eneo la Ajali ya Machi 10, 2019 karibu na Bishoftu, Ethiopia, siku mbili baada ya ajali mbaya ya Boeing 737 MAX 8 ya shirika la ndege la Ethiopia Airlines.
Eneo la Ajali ya Machi 10, 2019 karibu na Bishoftu, Ethiopia, siku mbili baada ya ajali mbaya ya Boeing 737 MAX 8 ya shirika la ndege la Ethiopia Airlines. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo amesema ripoti ya awali, inatarajiwa kuwekwa wazi ndani baada ya siku 30 zijazo.

Ndege zote zilizoanguka ni aina moja, Boeing 737 Max 8 na tayari uchunguzi unaendelea nchini Ufaransa, kubaini mawasiliano yaliyokuwepo kabla ya kuanguka ili kufahamu kilichosababisha ajali hiyo.

Uongozi wa Boeing kampuni uliotengeza ndege hiyo umesema unaunga mkono uchunguzi, ili kufahamu kilichotokea.

Mbali na hil, siku ya Jumapili jamaa ndugu na marafiki wa abiria walioangamia katika ajali hiyo walikuwa na misa ya kuwakumbuka wapendwa wao katika Makanisa ya Coptic jijini Addis Ababa na Nairobi nchini Kenya.

Serikali ya Ethiopia imesema uchunguzi wa mabaki ya abiria walifariki katika ajali hiyo utachukua miezi sita lakini kwa familia zimepewa udongo kutoka eneo la ajali hiyo kuendelea na maziko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.