Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Familia kupewa udongo kwa ajili ya maziko nchini Ethiopia kufuatia ajali ya ndege

media Mabaki baada ya kutokea kwa ajali ya ndege Boeing 737 nchini Ethiopia REUTERS/Baz Ratner

Wafanyikazi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa nchini Ethiopia wamekusanyika Jumapili,  kuwakumbuka wahudumu waliokuwa katika ndege ya abiria Boeing 737 MAX 8  iliyoanguka Jumapili iliyopita na kusababisha vifo vya watu  wote 157.

Wakiwa wenye huzuni na wakiangua vilio, wafanyikazi hao wameonekana wakiwa na mashada ya maua lakini pia mishumaa kama ishara ya kuwakumbuka wenzao.

Makanisani, ibada za kuwakumbuka raia wa nchi hiyo waliopoteza maisha pia imefanyika huku viongozi wa dhehebu la Coptic, wakionekana kuwatia moyo, jamaa ndugu na marafiki walioshindwa kujizuia, wakikumbuka kuondokewa na wapendwa wao.

Nayo serikali ya Ethiopia imesema familia zilizopoteza wapendwa wao, zitakabidhiwa mfuko wa udongo kutoka katika eneo lililotokea ajali hiyo kwa ajili ya mazishi kwa sababu, hakuna mwili uliopatikana.

Aidha, imesema familia zitapokea mabaki ya wapendwa wao baada ya uchunguzi ambao unatarajiwa kuchukua muda wa miezi sita.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana