Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-HAKI

DRC: Firmin Yangambi na Franck Diongo waachiliwa huru kwa msamaha wa Félix Tshisekedi

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)Felix Tshisekedi amesaini sheria za kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa na wale waliozuliwa kwa kutoa maoni yao.

Mwanasaiasa wa upinzani Franck Diongo Januari 12, 2015 Kinshasa, DRC.
Mwanasaiasa wa upinzani Franck Diongo Januari 12, 2015 Kinshasa, DRC. © PAPY MULONGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Sheria hizo zilisomwa kwenye televisheni ya serikali, Jumatano, Machi 13, na kuthibitishwa na mkurugenzi katika ofisi ya rais.

Firmin Yangambi na Franck Diongo ni miongoni mwa wanasiasa walioachiliwa huru kwa msamaha wa rais Felix Tshisekedi. Mkurugenzi katika ofisi ya rais Vital Kamerhe amesema kuwa huo ni mwanzo tu wa hatua. Firmin Yangambi na Franck Diongo walikuwa miongoni mwa kesi kubwa za wafungwa wa kisiasa ambao upinzani ulikuwa ukiomba ukisisitiza kuachiliwa huru tangu mwaka 2016.

Kwa mujibu wa Vital Kamerhe wafungwa takribani 700 ndio wanahusika na hatua hiyo ya rais nchi nzima.

Jina la tatu limeonekana kwenye orodha hii, ni lile la Eugene Diomi Ndongala, kiongozi wa chama kimoja cha upinzani kiliokuwa na uhusiano wa karibu na Etienne Tshisekedi. Diomi Ndongala anatarajiwa kuachiliwa huru kwa dhamana, baada ya aliyekuwa waziri wa sheria Alexis Thambwe kusaini waraka unaomwaachilia huru, kwani bado kuna utaratibu ambao unatakiwa hufuatwa.

Hata hivyo familia ya Eugene Diomi Ndongala imepokea hatua hiyo kwa shingo upande.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.