Pata taarifa kuu
DRC-YUMBI-MAUAJI-USALAMA

Umoja wa Mataifa: Mauaji ya Yumbi yalipangwa na ni uhalifu dhidi ya binadamu

Machafuko yaliyotokea katika eneo la Yumbi ni sawa na uhalifu dhidi ya binadamu, Umoja wa Mataifa umebainisha katika ripoti yake iliyotolewa Jumatatu, Machi 12.

Nyumba iliyochomwa moto katika wilaya ya Yumbi nchini DRC.
Nyumba iliyochomwa moto katika wilaya ya Yumbi nchini DRC. RFI/Patient LIGODI
Matangazo ya kibiashara

Yumbi ni wilaya ya mkoa wa Mai-Ndombe nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo katikati mwa mwezi Desemba, kabla tu ya kufanyika Uchaguzi Mkuu kulitokea mashambulizi mabaya yaliyosababisha vifo vya watu 535 upande wa jamii ya Banunu.

Machafuko ya kikabila yalitokea pia wakati jamii moja ilipotaka kuzika mmoja ya viongozi wao wa Kitamaduni katika ardhi ya jamii nyingine.

Aidha uchunguzi huo umeonesha pia vurugu zinaweza kuibuka tena wakati wowote.

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamefahamisha kuwa ghasia zilizotokea kati ya Desemba 16 na 18 zilikuwa zimepangwa.

Jamii ya kabila la Batende walivamia na kushambulia vijiji vya wa Banunu, na watu wachache tu ndio waliofanikiwa kutoroka.

Taarifa hiyo, imeongeza pia mamlaka katika eneo la Yumbi, kwenye jimbo la Mai-Ndombe, magharibi mwa nchi, zilishindwa kuwajibika kwa kuwalinda raia.

Timu hiyo ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa iliweza kuvifikia vijiji vitatu kati ya vinne, wakati wa mashambulizi yalipopamba moto.

Miili ya watu inaaminika pia ilitupwa katika mto Congo.

Ripoti hiyo imesema takriban watu 500 waliuawa ikiwemo familia kuchomwa moto ndani ya nyumba zao na mtoto wa miaka miwili kutupwa ndani ya tanki la maji machafu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.