Pata taarifa kuu
BURUNDI-MELCHIOR NDADAYE-MAUAJI-SIASA

Buyoya aitaka jamii ya kimataifa kuingilia mchakato wa maridhiano ya Burundi

Raisi wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya ameitaka jamii ya kimataifa kuingilia kati mchakato wa makubaliano ya amani kuhusu Burundi.

Raisi wa zamani wa Burundi Melchior Ndadaye
Raisi wa zamani wa Burundi Melchior Ndadaye ANP/AFP Dabrowski
Matangazo ya kibiashara

Buyoya anakabiliwa na hati ya kukamatwa,ambayo pia inatajwa kuwa moja ya ukiukwaji wa makubaliano ya Arusha ya mwaka 2000 yaliyokomesha mauaji ya kikatili nchini Burundi.

AFP imeshuhudia barua ya Buyoya ikionya juu ya kukwamishwa kwa mchakato wa maridhiano ya Warundi.

Barua hiyo ya March 1 iliandikwa kwa raisi wa Uganda Uganda Yoweri Museveni, ambaye alisimamia mkataba wa amani vilevile kwa Afrika kusini, Kenya, Rwanda, Tanzania, Umoja wa mataifa na umoja wa Ulaya.

Mnamo mwezi Novemba, Burundi ilitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa Buyoya,maafisa wengine 11 wa zamani na raia 5 walioko karibu nae kwa kuhusika na mauaji ya raisi wa zamani Melchior Ndadaye mnamo mwaka 1993.

Buyoya ni muwakilishi wa umoja wa Afrika nchini Mali anayeheshimiwa barabi na nje.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.