Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Ulimwengu waadhimisha siku ya wanawake duniani

media Siku ya wanawake duniani inaadhimishwa wakati wanawake wengi wanakabiliwa na hali duni ya maisha huku wengine wakilazimika kukimbilia katika makambi ya wakimbizi kutoka na na migogoo ya kisiasa. ©HCR/Corentin Fohlen

Leo Ijumaa Machi 8 ni siku ya Kimataifa ya Wanawake, siku ambayo dunia inathamini mchango wa wanawake katika jamii na kauli mbiu ya mwaka huu ni kuwapa wanawake na wasichana nafasi ya kuja na sera ya huduma mbalimbali zitakazosaidia kubadilisha maisha ya watu.

Hata hivyo, wanawake barani Afrika wameendelea kulalamika ubaguzi na uonevu katika masuala mengi hasa uongozi.

Kila mwaka wa tarehe 8 mwezi Machi,wanawake hukumbukwa kwa kuwa huwa ni siku iliyotengwa kwa ajili yao.

Kwa mujibu wa mwanamke mmoja aliyehojiwa na idhaa ya Kiswahili ya RFI mjini Bujumbura nchini Burundi, wanawake wanatambulika kuwa watu muhimu zaidi katika jamii.

“Jamii inayompuuza mwanamke katika shughuli za kimaendeleo huwa ni jamii isiyo na ustaarabu. Mwanamke akihusishwa katika shughuli za maendeleo ya jamii husaidia kuinua jamii hiyo na kuonekana ustaarabu katika jamii husika, “ amesema mwanamke huyo ambaye hakutaja jina lake.

“Mwanamke akiwekwa mstari wa mbele katika jamii basi husaidia katika kuendelea mbele kwa jamii hiyo. Wanawake husaidia katika uzalishaji wa jamii. Haki za wanawake hazifai kuwekwa kando na tathmini ya haki za binadamu” ameongeza.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana