Pata taarifa kuu
UFARANSA-AFRIKA-USHIRIKIANO

Rais wa Ufaransa kuzuru nchi za Pembe ya Afrika

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajia kuanza ziara ndefu barani Afrika ambapo ataanzia nchini Djibouti Machi 11 kabla ya kuelekea nchini Ethiopia Machi 12 na baadaye nchini Kenya.

Emmanuel Macron wakati wa ziara yake Ouagadougou (Burkina Faso) Jumanne, Novemba 28, 2017, alizungumza na umati wa wanafunzi. Atafanya atafanya hivyo katika Chuo Kikuu cha Nairobi (Kenya).
Emmanuel Macron wakati wa ziara yake Ouagadougou (Burkina Faso) Jumanne, Novemba 28, 2017, alizungumza na umati wa wanafunzi. Atafanya atafanya hivyo katika Chuo Kikuu cha Nairobi (Kenya). © REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Masuala ya kimkakati, kiuchumi, kiutamaduni na hali ya hewa ndivyo vilivyowekwa kwenye orodha ya ziara hii ya kwanza ya rais huyo katika Pembe ya Afrika.

Hatua ya kwanza ya ziara hii ilitangazwa kwa kuchelewa. Emmanuel Macron ataanza safari yake ya Machi 11 nchini Djibouti ambako atakuwa na kikao na rais wa nchi hiyo Ismaïl Omar Guelleh kabla ya kuzuru kambi ya wanajeshi wa Ufaransa ambayo inajumuisha idadi kubwa ya wanajeshi wa Ufaransa nje ya taifa hilo

Hii ni ziara ya kimkakati nchini Djibouti kutokana na kwamba nchi hiyo inapokea vituo vya kijehi kutoka katika mataifa makubwa yenye nguvu duniani kama vile (Marekani, Japan, Ujerumani, Italia na hivi karibuni China) - na ni mshirika mkubwa wa kihistoria, hivyo kulikuwa na umuhimu kuandaa ziara hiyo.

Emmanuel Macron atakuwa ni rais wa pili wa Ufaransa, baada ya Nicolas Sarkozy mwaka 2010, kwenda nchini Djibouti baada ya miaka ishirini. Ishara ya joto la mahusiano kati ya nchi hizo mbili, baada ya kutetereka mara kwa mara.

Wataalamu wanasema ziara hiyo inalenga kuonyesha uungwaji mkono kwa mshirika wa karibu wa Ufaransa kipindi hiki ambacho mshirika huyo hayupo katika wakati mzuri.

Jambo jingine linaelezwa kuwa ziara hiyo ni ya kimkakati kutokana na kwamba Ufaransa inatiwa wasiwasi na China ambayo imekuwa na ushawishi mkubwa katika eneo hilo, ambapo hivi karibuni wabunge wa Ufaransa walizuru nchini Djibouti na kugundua kwamba ushawishi wa Ufaransa umepungua pakubwa. Baada ya Djibouti rais Macron ataelekea nchini Ethiopia katika mji wa Lalibela kabla ya kutamatisha ziara yake nchini Kenya ambapo atakuwa ni rais wa kwanza wa Ufaransa kuzuru nchi hiyo, koloni ya zamani ya Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.