Pata taarifa kuu

Muhula wa 5 wa Bouteflika: Algeria yaendelea kukumbwa na maandamano

Maandamano yameendelea kupamba moto nchini Algeria ambapo Jumatano waandamanaji wamejitokeza kwa wingi katika maandamano mapya kupinga muhula wa 5 wa rais Aldelaziz Bouteflika, ambae hata hivyo hali yake ya afya inaelezwa kuwa tete tangu alipolazwa katika Hospital moja nchini Uswisi.

Maandamano dhidi ya muhula wa tano wa rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika, Algiers, Machi 3, 2019.
Maandamano dhidi ya muhula wa tano wa rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika, Algiers, Machi 3, 2019. REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Jumatano wiki hii, kambi ya AldelAziz Bouteflika imepata pigo kubwa baada ya kukosa uungwaji mkono wa chama cha Moudjahidine, cha wapiganaji wa zamani wa vita vya ukombozi, ambacho kimetangaza kuungana na waandamanaji.

Februari 12, Chama hicho kilikuwa kimetangaza kumuunga mkono Bouteflika, lakini hivi majuzi kimebadili msimamo na kueleza kwamba taasisi zilizopo nchini humo hazikidhi mahitaji ya wananchi.

Nchini Ufaransa katika kipindi cha maswali na majibu bungeni, waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean Yves Ledrian amesema wananchi wa Algeria ndio pekee wataoamuwa nani wa kuwaongoza.

Katika maandamano ya utulivu kupinga muhula wa 5 wa rais Abdelaziz Bouteflika ya Jumatano wiki hii, watu kadhaa walikamatwa.

Leo Alhamisi mawakili jijini Algiers wamepanga kuandamana hadi ofisi za mahakama ya kikatiba, huku Chama cha Umoja wa Mawakili nchini humo kikiitisha mgomo wa siku 4 kuanzia Machi 11.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.