Pata taarifa kuu
NIGERIA-BUHARI-UCHAGUZI-SIASA

Wanigeria wasubiri kuona hatua za Buhari

Baada ya kupiga kura na kumchagua rais wao Muhammadu Buhari kwa muhula mwingine wa miaka minne, wananchi wa Nigeria wanasubiri ahadi rais wao alizozitoa kama zitatekelezwa.

Watu wakikusanyika mbele ya duka la kuuza magazeti baada ya uchaguzi wa urais kuahirishwa Nigeria, Februari 16 Lagos.
Watu wakikusanyika mbele ya duka la kuuza magazeti baada ya uchaguzi wa urais kuahirishwa Nigeria, Februari 16 Lagos. © REUTERS/Temilade Adelaja
Matangazo ya kibiashara

Muhammadu Buhari mwenye umri wa miaka 76 alichaguliwa kwa muhula wa pili. Mwaka 2015, kuchaguliwa kwake kulifufua matumaini mengi, na kuonyesha ishara ya kupishana kwenye madaraka kwa njia ya kidemokrasia. Leo, kuchaguliwa kwake kwa muhula wa pili kunaonekana kama chanzo cha utulivu, hata kama matokeo ya sera yake yamekuwa yakikosolewa na wengi.

Atiku Abubakar, ambaye alichukuwa nafasi ya pili katika uchaguzi huo wa urais kwa 41% ya kura, amepinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi (INEC). Kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha PDP anashtumu INEC kubadilisha matokeo ya uchaguzi kwa niaba ya Muhammadu Buhari.

"Siku ya uchaguzi, tulishuhudia mpango uliowekwa ili kuiba haki ya kujieleza ya wananchi. Tuliona mambo ambayo hayawezekani. Kwa mfano, katika Jimbo la Borno, kiwango cha ushiriki kilikuwa kikubwa: kiwango hicho kilifikia kimiujiza 82%, wakati kunaripotiwa mdororo wa usalama. Hali hii ilishuhudiwa hata katika majimbo kadhaa ambayo Chama cha Congressist kilisinda. Raia wenzangu, ndiyo sababu mimi, Atiku Abubakar, nimepinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ... Na ninatangaza kwamba Muhammadu Buhari alichaguliwa kwa kura nyingi zisizo halali", amesema Atiku Abubakar, kiongozi wa chama cha upinzani cha PDP.

Hata hivyo Atiku Abubaka amesema atafikisha malalamiko yako mbele ya mahakama.

Baada ya kutangazwa mshindi, rais Muhammadu Buhari aliwashukuru waliompigia kura na wale ambao waliwezesha kufanyika kwa uchaguzi.

Wakati huo huo alisema kazi kubwa anayotarajiwa kufanya katika muhala wake wa miaka minne ijayo.

"Utawala mpya utaongeza juhudi zake katika njanya ya usalama, kufufua uchumi na kupambana na rushwa. Tumeweka mambo yote sawa na tutafanya kinachowezekana kwa mabadiliko muhimu. Pia tutapambana ili kuimarisha umoja wa nchi yetu na kushirikisha wote ili kundi au chama chochote kijisikie kimetengwa. Ninawashukuru kuniunga mkono. Mungu aibariki Jamhuri ya Nigeria", alisema Muhammadu Buhari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.