Pata taarifa kuu
SENEGAL-SIASA-UCHAGUZI

Senegal: Chama tawala na upinzani watoa misimamo tofauti, zoezi la kuhesabu kura laendelea

Siku moja baada ya wananchi wa Senegal kupiga kura, waziri mkuu wa nchi hiyo amedai kuwa mgombea wao Macky Sall ameshinda uchaguzi huo.

Wananchi wa Nigeria wakipiga kura, kumchagua rais wao mpya.
Wananchi wa Nigeria wakipiga kura, kumchagua rais wao mpya. © Carmen Abd Ali / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea nchini Senegal, mvutano umeanza kujitokeza kati ya pande zilizowania katika uchaguzi huo, baada ya waziri mkuu kutangaza kwamba rais anaye maliza muda wake Macky Sall ameshinda uchaguzi huo.

Wakati huo huo Tume ya Uchaguzi inaendelea kukusanya matokeo ya uchaguzi kutoka vituo vya kupigia kura 16,000 nchini kote.

Tayari upinzani na vyama vinavyomuunga mkono rais anaye maliza muda wake. Macky Sall, wametoa msimamamo yao ambayo imetofautiana kabisa.

Jumapili jioni, Idrissa Seck, mmoja wa wagombea wa upinzani aliwasili katika ngome yake ya Thiès, akiwa pamoja na Ousmane Sonko, mgombea mwengine wa upinzani anayewania kiti cha urais. Bila kutaja kura alizopata, kiongozi huyo wa chama ch Rewmi alitoa wito kwa wafuasi wake kujiandaa kwa duru ya pili ya uchaguzi kwa utulivuhuku akishtumu chama tawala kutaka kuiba kura. "Kwa hiyo tunakuja kusema kwa uwazi kwamba katika hatua hii, tunajiandaa katika duru ya pili ya uchaguzi na matokeo ambayo tayari yamekusanywa yanaturuhusu kusema hivyo. "

"Ninatoa wito kwa viongozi wa kidini kuomba chama tawala kukubali matokeo," amesema kwa upande wake kiongozi wa chama cha Pastef, Ousmane Sonko, ambaye aliwasili katika ngome yake ya Ziguinchor.

Jumapili jioni vyombo vya habari vilibani kwamba Macky Sall, Idrissa Seck na Ousmane Sonko wanaongoza katika uchaguzi huo na huenda wakapambana katika duru ya pili ya uchaguzi.Hata hivyo Idrissa Seck na Ousmane Sonko wameamua kufanya muungano wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.