Pata taarifa kuu
ALGERIA-SIASA-URAIS

Abdelaziz Bouteflika kuwania urais kwa muhula wa tano

Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika atawania urais kwa muhula wa tano wakati Uchaguzi Mkuu utakapofanyika nchini humo mwezi Aprili.

Rais wa Algeria  Abdelaziz Bouteflika
Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika RYAD KRAMDI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limetolewa na Shirika la Habari la taifa nchini humo APS, ambalo limethibitsiha kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 81 na ambaye amekuwa rais tangu mwaka 1999, atateta wadhifa wake.

Tangu mwaka 2013, rais Bouteflika, amekuwa akitumia gari la magudumu baada ya kupata kiharusi.

Mara nyingi rais Bouteflika, huwa haonekani hadharani baada ya kupata changamoto hii ya kiafya.

Watu wake wa karibu wanasema hali yake ya kiafya sio kigezo cha raia huyo kutowania urais, kwa sababu chake kimeonesha imani ya kutaka aendelee kuongoza.

Licha ya ukosoaji mkubwa kwa kutotaka kuondoka madarakani, rais Bouteflika anayetambuliwa pia kwa kuvalia suti, licha ya joto na jua hali, anakumbukwa kwa kusadia nchi yake kumaliza vita vya wenyewe kwa wenywe vilivyosababisha vifo vya zaidi ya watu 200,000 kabla ya kuingia madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.