Pata taarifa kuu
EAC-AFRIKA-HAKI

Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Ukeketaji wa Wanawake na Watoto wa kike yaadhimishwa

Tarehe 6 Februari kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kupinga Ukeketaji duniani kote. Historia ya siku hii ilianza mwaka 2003 ambapo Baraza la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kuwa siku rasmi ya kimataifa ya kupinga Ukeketaji duniani kote.

Msumari uliotengenezwa kienyeji ni moja ya vifaa vinavyotumiwa katika kukeketa wanawake na watoto wa kike katika baadhi ya jamii Afrika. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa wanawake zaidi ya milioni 200 na wasichana wamekeketwa dunia.
Msumari uliotengenezwa kienyeji ni moja ya vifaa vinavyotumiwa katika kukeketa wanawake na watoto wa kike katika baadhi ya jamii Afrika. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa wanawake zaidi ya milioni 200 na wasichana wamekeketwa dunia. AFP/Yasuyoshi Chiba
Matangazo ya kibiashara

Baraza la Umoja wa Mataifa lilifikia uamuzi huu baada ya kutathimini na kuona athari kubwa zitokanazo na vitendo vya ukeketaji kwa mtoto wa kike.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, yanapinga vikali ukeketaji dhidi ya wanawake.   Zaidi ya wanawake na wasichana milioni mia mbili wamekeketwa duniani, huku nusu yao wakiishi Misri, Ethiopia, Indonesia. Nchi za Somalia, Guinea na Djibouti zikionyesha idadi kubwa ya wanawake waliokeketwa Barani Afrika.

Wakati Dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya kumaliza kabisa vitendo vya ukeketaji na kufikia sifuri, Umoja wa Mataifa unafanya kazi ya kuhakikisha kwamba mila hizi zinakoma mpaka kufikia mwaka 2030, mkakati uliotengwa kwenye Maendeleo endelevu ulio idhinishwa na Baraza la Umoja wa Mataifa mwezi September, mwaka jana.  Kati ya watu milioni mia mbili waliokeketwa, Milioni 44 ni wasichana walio chini ya umri wa miaka 14  au wadogo zaidi ya hapo.  Katika nchi 30 duniani ambako vitendo hivi vinaendelea kutekelezwa, wasichana wengi  wamefanyiwa ukeketaji hata kufikia miaka mitano ya kusherehekea siku yao ya kuzaliwa.  Vitendo hivi ni wazi vinavunja Haki za Watoto.

UNICEF imesema kuwa kwenye nchi za Somalia, Guinea na Djibouti, mila ya ukeketaji ni kama imekubalika nchi nzima.  Vitendo hivi vimepungua sana katika nchi za Liberia, Burkina Faso, Kenya na Misri. Ambako hatua kubwa imepigwa kupinga mila hii.  Nchi tano zimepitisha sheria kali na kufanya vitendo vya ukeketaji  kuwa ni kosa la jinai.  Nchi hizoni pamoja na Kenya, Uganda na Guinea Bisau.   Na hivi karibuni nchi za Nigeria na Gambia pia zimepitisha sheria hiyo mwaka 2017.

Ukeketaji ni kitendo cha kukata, kuvuta ama kuharibu kwa namna yoyote ile kiungo cha ndani au cha nje cha uke wa mtoto wa kike. Tendo hili hufanywa pasipokuwa na sababu zozote za kisayansi/kiafya. Ni kitendo kinachomdhalilisha mtoto wa kike na kumwondolea utu wake kama mwanandamu aliyeumbwa kamili. Historia ya utekelezaji wa mila hii potofu inasadikika kuanza yapata miaka 2000 iliyopita. Ukeketaji mara zote hufanyika kwa sababu ya misukumo ya kibinadamu, ikiwemo kupata mali kwa kumwozesha binti aliyekeketwa, kutii masharti ya mila kama ya kutambika mizimu, kuondoa mikosi katika familia, kumvusha mtoto rika na nyinginezo nyingi. Hata hivyo sababu hizo zote hazina maana zaidi ya kuendeleza tamaduni kandamizi kwa wanawake na watoto wa kike.

Kwa mujibu wa Daktari Beatrice Kamikazi wa hospitali ya Hyppocrate mjini Bujumbura yapo madhara mengi yanayosababishwa na ukeketaji; madhara hayo yanaweza kuwa ya kiafya au hata kisaikolojia.

“Madhara yanayosababishwa na ukeketaji yanaweza kuwa ya papo kwa papo kama maumivu makali wakati wa ukeketaji, mshtuko, homa kali, kumwaga damu nyingi na mara nyingine hata kupelekea kifo, kuambukizwa magonjwa kama Virusi Vya UKIMWI na msongo wa mawazo. Yapo pia madhara ya muda mrefu kama vile; kuathirika kisaikolojia, ulemavu/kovu la kudumu katika uke, fistula, kupata shida wakati wa kujifungua na muda mwingine kupelekea kupata ugumba, “ amesema Dkt kamikazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.