Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Mashambulizi ya Boko Haram yaua watu sita

Watu sita wameuawa katika mashambulizi kadhaa yaliyotekelezwa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. 

Mazishi ya mmoja wa wakulima waliouawa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram huko Kalle, kilomita 17 kutoka Maiduguri Oktoba 20, 2018.
Mazishi ya mmoja wa wakulima waliouawa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram huko Kalle, kilomita 17 kutoka Maiduguri Oktoba 20, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji wa kundi hilo waliipora biashara na kuzingira vijiji kadhaa, vyanzo vya serikali ya mitaa vimebaini.

Siku ya Jumatatu wapiganaji wa kundi la Abubakar Shekau walivamia vijiji vya Shuwa na Kirkina katika wilaya ya Madagali kaskazini mashariki mwa Adamawa.

"Wapiganaji wa Boko Haram waliua mtu mmoja huko Shuwa na wengine wawili huko Kirkina," Maina Ularamu, kiongozi wa jamii moja huko Adamawa ameliambia shirika la Habari la AFP.

"Magaidi" walimshambulia Shuwa karibu saa 12:45 jioni, huku wakirusha risasi na grunedi, "Maina Ularamu amesema, akibainisha kuwa polisi walikuwa walitoroka wilaya hiyo.

Wapiganaji waliiba magari na wkupora biashara kabla ya kuchoma moto nyumba kadhaa.

Askari wa Nigeria wanaopiga kambi huko Madagali, kilomita 13 na maeneo ya tukio, waliingiulia kati na kuwatimua wapiganaji hao, ambao walitimkia katika msitu wa Sambisa, ngome yao.

Saa chache kabla, kundi hilo liliua wachungaji watatu huko Tubba nje kidogo ya jiji la Maiduguri, mji mkuu Jimbo jirani la Borno.

"Tumepata miili ya wachungaji watatu katika mashamba," amesema Umara Kyari, mwenyeji wa kijiji jirani.

"Wachungaji wengine wawili waliokuwa pamoja nao walitoweka au walitekwa nyara na washambuliaji," amesema Mustapha Muhammad, mmoja wa wanamgambo wanaopigana kwa upande wa jeshi la Nigeria.

Boko Haram imeongeza mashambulizi yake dhidi ya wakulima, ikiwashtumu kutoa taarifa kwa jeshi.

Watu zaidi ya 27,000 wameuawa tangu kundi la Boko Haram kuanza mashambulizi yake Kaskazini-Mashariki mwa Nigeria mnamo mwaka 2009, huku watu milioni 1.8 wameshindwa kurudi makwao kutokana na usalama mdogo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.