Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-UBELGIJI-GBAGBO-ICC-HAKI

ICC yamkabidhi Laurent Gbagbo kwa mamlaka ya Ubelgiji

Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo ameondoka Uholanzi tangu Jumanne jioni na tayari amewasili nchini Ubelgiji. Laurent Gbagbo ambaye alifutiwa mashitaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu tarehe 15 Januari, aliachiwa huru tarehe 1 Februari.

Laurent Gbagbo, rais wa zamani wa Cote d' Ivoire, wakati kesi yake ikisikilizwa ICC, tarehe 15 Januari 2019.
Laurent Gbagbo, rais wa zamani wa Cote d' Ivoire, wakati kesi yake ikisikilizwa ICC, tarehe 15 Januari 2019. © CPI
Matangazo ya kibiashara

Waendesha mashitaka wa ICC wamesema wanapanga kukataa rufaa uamuzi huo wa majaji kumuachia huru Gbagbo.

Laurent Gbagbo aliondoka nchini Uholanzi, akisindikizwa na maofisa wa usalama wa ICC kabla ya kukabidhiwa kwa mamlaka ya Ubelgiji muda mfupi kabla ya saa nne usiku Jumanne wiki hii.

Hata hivyo Gbagbo amepewa masharti kuwa atakuwa katika nchi ambayo itakubali kumpa hifadhi na ataweza kurejea katika mahakama hiyo iwapo atahitajika kufanya hivyo.

Gbagbo ambaye alikuwa gerezani kwa miaka saba, alikuwa rais wa Cote d' Ivoire kati ya mwaka 2000 na 2011.

Alifikishwa katika mahakama ya ICC kwa mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu baada ya machafuko ya baada ya uchaguzi kuzuka nchini mwake mwaka 2011 kufuatia kukataa matokeo ya kushindwa katika uchaguzi ambapo watu zaidi ya 3,000 waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.