Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

CAR: Serikali na makundi 14 ya waasi watia sahihi mkataba wa amani Khartoum

media Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na shughuli za Amani, Kamishna wa Umoja wa Amani anaye husika na masuala ya Usalama na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan katika kikao cha ufunguzi wa mazungumzo huko Khartoum tarehe 24 Januari 2019. ASHRAF SHAZLY / AFP

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na makundi kumi na nne ya waasi wametia sahihi kwenye mkataba wa amani uliofikiwa baada ya siku kumi ya mazungumzo chini ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

Hakuna anayejua kwa wakati huu yaliyomo kwenye mkataba huo.

Mengi huenda yakajulikana wakati wa kusainiwa kwa mkataba huo mjini Bangui katika siku chache zijazo.

Mkataba mpya wa amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na makundi 14 ya waasi umetiliwa saini katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum. Sherehe hiyo ilifanyika mbele ya rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadera na rais wa Sudan Omar al-Bashir, pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat.

Rais wa Chad alikuwa anatarajiwa, lakini hakuweza hakuweza kuwasili jijini Khartoum kwa sababu ya mkutano wa G5 Sahel uliopangwa kufanyika nchini Burkina Faso.

Makundi ya watu wenye silaha yanadhibiti karibu asilimia 80 ya nchi hiyo , makubaliano haya mapya - ambayo ni ya nane sasa- yameleta matumaini mapya kwa wananchi wa taifa hilo, hata kama kwa sasa hayajawekwa wazi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana