Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika
CAR

CAR: Sherehe ya kutiwa saini kwenye mkataba wa amani yaahirishwa

media Jean-Pierre Lacroix (kushoto) Mkuu wa shughuli za amani za Umoja wa Mataifa na Smaïl Chergui (katikati), kamishna wa amani na usalama wa Umoja wa Afrika wakati wa mazungumzo huko Khartoum. ASHRAF SHAZLY / AFP

Sherehe iliyokuwa imepangwa kufanyika Jumapili katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, kuhusu makubaliano ya amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imeahirishwa.

Makundi 14 ya waasi yaliyowakilishwa katika mazungumzo na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yalitarajia kutia saini kwenye mkataba walioafikiana Jumamosi wiki hii iliyopita.

Hata hivyo makundi yote yameelezea furaha yao baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo mjini Khartoum.

Baada ya siku kumi ya mazungumzo, siku ya Jumamosi Umoja wa Afrika ulitangaza kwamba makundi ya waasi na Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wamefikia makubaliano. Kila upande umeridhia, lakini bila kutoa maelezo.

Makundi ya watu wenye silaha yanadhibiti karibu asilimia 80 ya nchi hiyo , makubaliano haya mapya - ambayo ni ya nane sasa- yameleta matumaini mapya kwa wananchi wa taifa hilo, hata kama kwa sasa hayajawekwa wazi.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, mkataba huo unazungumzia masuala nyeti kama msamaha kwa makundi ya waasi, kuundwa kwa serikali ya umoja, wapoganaji kutoka makundi mbalimbali kuingizwa katika vikosi vya usalama na ulinziu, na kutafutia suluhu matatizo mengine yanayuikabili nchi hiyo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana