Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-GBAGBO-ICC-HAKI

Hatma ya Laurent Gbagbo na msaidizi wake wa zamani kujulikana Ijumaa hii

Hatima ya kesi inayomkabili aliyekuwa rais wa Icote d'Ivoire Laurent Gbagbo pamoja na msaidizi wake Charles Ble Gude hatimaye itajulikana hii leo Ijumaa, katika mahakama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC).

rais wa zamani wa cote d'Ivoire Laurent Gbagbo.
rais wa zamani wa cote d'Ivoire Laurent Gbagbo. ICC/CPI
Matangazo ya kibiashara

Majaji wa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wanatazamiwa kukutana hii leo ijumaa wiki mbili baada ya Kitengo cha rufaa cha Mahakama hiyo kuagiza kuendelea kuzuiliwa jela kwa rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo na waziri wake wa zamani Charles Blé Goudé.

Kitengo cha rufaa cha Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kiliichukuwa uamuzi huo kufuatia hatua ya Mwendesha mashitaka wa ICC kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ambao January 15 walimfutia mashitaka Gbagbo na msaidizi wake wa zamani na kuamuru waachiliwe huru.

Fadi El Abdallah, msemaji wa ICC amesema uamuzi huu wa kitengo cha rufaa cha Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kuendelea kumzuia Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude umechukuliwa na majaji watatu kati ya watano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.