Pata taarifa kuu
THIOPIA-DJIBOUTI-WAHAMIAJI-USALAMA

Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya boti yaongezeka hadi 47

Wahamiaji zaidi ya 100 wametoweka na wengine zaidi ya 47 wamepatikana wamekufa maji baada ya boti mbili walizokuemo kuzama katika pwani ya Djibouti, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza.

Zoezi la kuwatafuta manusura wa ajali ya boti mbili kwenye Pwani ya Godoria, Djibouti, linaendelea, Januari 29, 2019.
Zoezi la kuwatafuta manusura wa ajali ya boti mbili kwenye Pwani ya Godoria, Djibouti, linaendelea, Januari 29, 2019. © International Organization for Migration / AFP
Matangazo ya kibiashara

Boti mbili zilizobeba raia wa Ethiopia zilizama muda mfupi baada ya kuondoka Djibouti mawimbi makubwa yalikuwa yakivuma baharini, amesema Lalini Veerassamy, mkuu wa ujumbe wa IOM nchini Djibouti.

kikosi cha ulinzi katika pwani ya Djibouti kinaendelea zoezi la kutafuta watu waliotoweka kwa matumaini ya kuwapata watu ambao bado hai.

Wahamiaji wengi kutoka nchi za Afrika wamepoteza maisha wakijaribu kuvuka bahari kuelekea Ulaya.

Nchi za Ulaya zimekuwa zikijaribu kuzuia wimbi hilo la wahamiaji wanaoelekea Ulaya, bila mafanikio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.