Shirikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu limetoa tahadhari wakati nchi hiyo ikiadhimisha miaka nane ya maandamano makubwa yaliyoangusha utawala wa Hosni Mubarak Januari 25, 2011.
Kwa mujibu wa Amnesty, mamlaka ya Misri ilikamatwa watu takribani 113 mwaka 2018 kwa sababu "walitoa maoni yao kwa amani".
"Leo hii, ni hatari zaidi katika historia ya hivi karibuni ya Misri kuikosoa serikali," mkurugenzi wa Amnesty International katika eneo la Afrika kaskazini, Najia Bounaim amesema katika taarifa ya shirika hilo.
"Chini ya uongozi wa Rais Abdel Fattah al-Sisi, Misri imekuwa gereza kwa wapinzani," Amnesty International imesema.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na kituo cha habari cha Marekani cha CBS, Bw Sissi alikanusha madai kwamba Misri ina wafungwa wa kisiasa.
Serikali yakeimekuwa ikishtumiwa mara kwa mara na mashirika ya haki za binadamu yanayolaani ukandamizaji dhidi ya wanasiasa wa upinzani au wanasiasa wa mrengo wa kushoto hata kuwasaka wafuasi wa Kiislam wa Muslim Brotherhood, ambao sasa wamepigwa marufuku.
Mbali na kukamatwa kwa wanaharakati wa haki za binadamu, hivi karibuni Misri ilipitisha sheria kuruhusu mamlaka kufuatilia akaunti maarufu zaidi katika mitandao ya kijamii na kufunga kama mamlaka hizo zinaona kuwa mitandao hiyo inachapisha "habari za uongo."