Pata taarifa kuu
SUDAN-MAREKANI-USALAMA-USHIRKIANO

Washington yatoa wito kwa Sudan kuachilia huru waandamanaji

Marekani imetoa wito kwa serikali ya sudan kuanzisha uchunguzi wa watu waliouawa katika maandamano yaliyozuka hivi karibuni nchini humo na kuitaka kuawaachiliwa huru waandamanaji wanaozuiliwa.

Maandamano dhidi ya serikali katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, Desemba 25, 2018.
Maandamano dhidi ya serikali katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, Desemba 25, 2018. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Marekani imetoa kauli hiyo ikisema kuna uwezekano wa kurejesha uhusiano mzuri kati ya Khartoum na Washington.

Taarifa ya wizara ya mambo ya kigreni ya Marekani ni ya kwanza tangu kuanza kwa maandamano nchini Sudan Desemba 19. Maandamano hayo yalizuka kufuatia uamuzi wa serikali wa kuongeza mara tatu bei ya mkate. Maamdamano ambayo yalibadili mwelekeo na kuwa maandamano dhidi ya utawala wa Rais Omar al-Bashir, ambaye anaongoza nchi hiyo kwa mkono wa chuma tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1989.

Marekani imesema "ina wasiwasi na idadi kubwa ya watu wanaokamatwa na kufungwa" na imetoa wito kwa Sudan kuwaachilia huru "waandishi wa habari, wanaharakati na waandamanaji walioandamana kwa amani ambaowanazuiliwa kiholela".

"Pia tunatoa wito kwa serikali kuruhusu uchunguzi wa kuaminika na huru kwa watu waliouawa na waliojeruhiwa wakati wa waandamanaji," msemaji wa wizara ya mamabo ya kigeni ya Marekani, Robert Palladino amesema.

"Kwa kushughulikia malalamiko halali ya wananchi serikali inapaswa kujenga mazingira salama kwa weka mbele uhuru wa kujieleza na mazungumzo na upinzani pamoja na mashirika ya kiraia, katika kuendeleza mchakato wa kisiasa usiombagua yeyote", Robert Palladino amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.