Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Kiongozi wa zamani wa waasi wa Anti-balaka asafirishwa ICC

media Patrice Edouard Ngaissona, Waziri wa zamani wa Vijana na Michezo chini ya utawala wa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize, ni mratibu wa kisiasa wa makundi ya kijeshi ya Anti-Balaka. ISSOUF SANOGO/AFP/Getty

Mamlaka nchini Ufaransa imemkabidhi Patrice-Edouard Ngaïssona, kiongozi wa zamani wa wanamgambo wa Anti-balaka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Bw Ngaissona anashtumiwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ICC imesema katika taarifa yake.

Alikamatwa Desemba 12 kufuatia hati ya kukamatwa iliyotolewa na ICC "kwa kuhusika kwake kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanyika magharibi ya Jamhuri ya Afrika Kati ya Septemba 5, 2013 na mwezi Desemba 2014 ". Mahakama ya Ufaransa iliamuru Bw Ngaissona asafirishw mjini Hague.

Jamhuri ya Afrika ya Kati ilikumbwa na machafuko mnamo mwezi Machi 2013 baada ya utawala kudhibitiwa na waasi wa Kiislam wa Seleka na kufanyiwa upinzani wa kijeshi na wanamgambo wa Kikristo wa Anti-Balaka.

Hata hivyo Patrice-Edouard Ngaissona, ambaye amekanusha tuhuma hizo dhidi yake, alichaguliwa mwezi Februari kwenye kamati tendaji ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), licha ya upinzani kutoka mashirika ya haki za binadamu kama vile Human Rights Watch.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana