Jeshi la DRC laua wanamgambo saba Ituri
Wanamgambo sita na kiongozi wao wameuawa wakati wa operesheni ya kijeshi katika mkoa wa Ituri, Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), jeshi la DRC limesema katika taarifa yake.
Imechapishwa:
" Tumeshambulia ngome ya wanamgambo wa Mai-Mai Simba usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne na tumeuawa wanamgambo saba, ikiwa ni pamoja na kiongozi wao Manu", Luteni Jules Tshikudi, msemaji wa Jeshi la FARDC katika mkoa wa Ituri (kaskazini mashariki) ameliambia shirika la Habari la AFP.
Operesheni hiyo imefanyika katika eneo la Pembele, kilomita10 kutoka Nyanya katika wilaya ya Mambasa, magharibi mwa Bunia.
Taarifa hii ya kuuawa kwa wanamgambo saba imethibitishwa na Mkuu wa wilaya ya Mambasa Mambasa, Idris Lokodila.
"Wakazi wanafurahi kusikia kuwa Manu ameuawa, kiongozi wa waasi aliyetesa wananchi," Bw Lokodila amesem.
Manu, ambaye jina lake halisi halijulikani, alichukua mikoba ya Paul Sadala, kwa jina maarufu Morgan, ambaye aliuawa mnamo mwaka 2014.
anashtumiwa kuendesha ujangili katika hifadhi ya Okapi, eneo la Epulu.